Monday, 25 April 2016

Kauli ya Prof. Mbarawa kuhusu watumishi wazembe

 
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa wizara yake haitawavumulia watendaji wazembe na wasiotaka kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo hii leo alipotembealea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchiniTanzania (TMA) na kubainisha kuwa anawataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kuwatendea haki watanzania ambao kwa kiasi kikubwa wanawategemea wao kujua masuala mbalimbali yahusuyo hali ya hewa.

Aidha, Profesa Mbarawa amesema kuwa anaitaka mamlaka hiyo kuanzisha utaratibu wa kupima utendaji kazi wa wafanyakazi kwa mwaka mzima ambapo ndio kitakuwa kigezo cha kumpandisha daraja mfanyakazi au kumuongezea mshahara.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa ameitaka mamlaka ya hali ya hewa nchini kuachana na mfumo wa zamani wa kuhifadhi kumbukumbu zao kwa njia ya makaratasi na badala yake watumie njia ya komputa njia ambayo ni rahisi na inabana matumizi ya karatasi.

No comments:

Post a Comment