Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli ameiagiza mifuko ya hifadhi za jamii nchini kubadilisha aina ya uwekezaji badala ya kuendelea kuwekeza katika majengo badala yake waanze kuwekeza katika ujenzi wa viwanda
Rais amesema ni vyema viongozi na wataalamu waliopo katika mifuko ya hifadhi nchini kuanza kufikiria nje ya ukuta kwa kuanza kujenga viwanda ambavyo vitakuwa na manufaa makubwa kwa watanzania wengi hasa vijana ambao watapata ajira katika viwanda hivyo.
Amesema tofauti na ilivyo sasa pamoja na uwekezaji huo watu wachache wenye kipato kikubwa ndio wamekuwa wakimudu kukodi majengo hayo huku watanzania wengi masikini wakishindwa kumudu gharama za pango hivyo kufanya majengo hayo kukosa wapangaji.
Awali wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la PPF mjini Arusha lenye ghorofa 8 lililogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 33.91 waziri wa fedha Dakta Philip Mpango na waziri wa sera,bunge,kazi,ajira na watu wenye ulemavu Jenisther Mhagama wamewapongeza PPF kwa uwekezaji huo na kusema kuwa hakuna taifa lolote linaloweza kuendelea bila uwekezaji wa ndani na nje.
Nae mkurugenzi mkuu wa PPF William Erio amesema kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 mfuko umeanza mkakati wa miaka mitatu wa kutekeleza agizo la rais magufuli la kuwekeza katika viwanda vitakavyotumia malighafi inayopatikana hapa nchini.
No comments:
Post a Comment