Monday, 9 May 2016

Hii ndio nauli mpya iliyotangazwa na SUMATRA leo ya Mabasi yaendayo haraka.


Mradi wa mabasi yaendayo haraka Katika jiji la Dar es salaam unatarajiwa kuanza rasmi kesho, Yakianza safari zake kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa sita usiku, huku uongozi wa kampuni ya UDA -RT inayoendesha huduma ya usafiri wa mabasi hayo ukitoa fursa ya wananchi kupanda bure kwa siku mbili kuanzia kesho. IMG_8841 Mradi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu baada ya serikali yake kulazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo wa viwango vikubwa vya nauli, leo Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi kavu na Majini SUMATRA imetangaza rasmi viwango vya nauli zitakazotumika.

Kwa mujibu wa SUMATRA, Nauli toka Kimara hadi kivukoni itakuwa shilingi 650, kutoka Mbezi Mwisho hadi kivukoni itakuwa 800 na barabara za mwendo wa haraka za pembezoni nauli yake  itakuwa shilingi 400. Mwanafunzi atalazimika kulipa shilingi 200 kwa safari yeyote atakayoifanya.

Mbali ya Kutangaza nauli hizo, SUMATRA, imetoa leseni ya mwaka mmoja kwa Kampuni ya UDA RT ILI Kuendesha huduma hiyo ya usafiri katika jiji la Dar es salaam

No comments:

Post a Comment