Monday, 9 May 2016

Idadi ya watumishi hewa imefikia hii jijini Dar es salaam

 
Sakata la watumishi hewa katika jiji la dsm limeendelea kuchukua sura mpya baada ya kubainika watumishi hewa wengine 39

ikiwa ni siku saba tu tangu wakuu wa idara na maafisa utumishi wa manispaa za jiji la dsm kusaini mikataba inayobana ili kuanza uchunguzi wa kina kuhusu idara zao.

Kugundulika kwa watumishi hao katika awamu hii ya tatu ya Uchunguzi inafikisha watumishi hewa 248 katika jiji la dsm tangu rais magufuli kuwataka wakuu wa mikoa kuchunguza kwa kina juu ya kuwapo watumishi hao , ambao katika jiji la dsm mpaka sasa kiasi cha Shilingi bilion 3.636 zimepotea.

Katika kuonyesha Serikali imedhamiria kukomesha upotevu wa Fedha kutokana na watumishi hewa Mkuu wa mkoa wa dsm amemsimamisha kazi na kutaka Uchunguzi ufanyike Afisa Mtumishi mkuu wa manispaa ya Ilala Francis Kilawe baada ya kushindwa kujieleza kutokana na watumishi hewa 11 ambapo hawapo kazini,hawajulikani wako idara wala vitengo gani lakini wakipokea mishahara tangu 2010 huku afisa mtumishi mkuu akisaini na kuidhinisha mishahara yao.Aidha afisa Utumishi wa afya manispaa ya temeke Dr.Slylivia Mamkwe amesimamishwa ili kupisha uchunguzi.

Aidha baadhi ya wakuu wa idara na maafisa Utumishi wameomba kuongozewa wiki mbili zaidi ili kuwabaini watumishi hewa kwa madai kuwa wanaonekana katika mfumo wa kupokea malipo kutoka hazina kwenda katika manispaa

No comments:

Post a Comment