Monday 9 May 2016

HESLB yakusanya zaidi ya bil 4 kwa siku 30

Bw. Cosmas Mwaisobwa
Zaidi ya shilingi bilioni 4 zimekusanywa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), katika siku 30 za mwanzo walizozitoa kwa wanufaika wa mkopo kurejesha fedha wanazodaiwa na waajiri kupeleka majina ya waajiriwa.
 Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Bw. Cosmas Mwaisobwa, amesema kuwa muitikio ni mzuri kwani kwa siku wanapokea watu 80 hadi 100 wanaokwenda kuchukua fomu za kiasi wanachodaiwa huku jumla ya wahitimu 20,341 wametambuliwa kuwa wanadaiwa na bodi hiyo ya mikopo.

Aidha, Bw Mwaisobwa amesema kuwa kiasi cha pesa kinachokatwa na HESLB kila mwezi ni asilimia 8 ya mshahara wa mtu hivyo kiasi kitakachokatwa kitatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. 

Amesema zitakapokamilika siku 60 ndipo watakapofanya tathmini ya jumla kujua iadadi kamili ya wahitimu waliomaliza na wale wasiomaliza madeni yao.

No comments:

Post a Comment