Monday 9 May 2016

Mauaji ya Kutatanisha yatokea katika manispaa ya Songea

 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Masanja Aliko mfanyakazi wa machinjio ya ng’ombe Msamala manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ameuwawa katika mazingira ya kutatanisha na watu  wasiofahamika akiwa kwenye eneo lake la kazi.


Tukio hilo limetokea mei nane saa saba usiku katika machinjioni ya Msamala masanja alifika usiku huo kwaajili ya kupokea ngíombe waliokuwa wameletwa kutoka mkoani Mbeya mara baada ya kupokea ngíombe hao alirudi nyumbani muda mfupi baadae alisikika akilia na  kuomba msaada.

Ndugu wa marehemu wamesema kuwa wanamashaka kuwa alikimbizwa na akupigwa na polisi waliokuwa doria na kusababisha kifo chake na kwamba walipofuatilia kituo cha polisi waliambiwa hakuna taarifa ya kifo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Zubery Mwombeji amesema kuwa maelezo ya kifo cha Masanja yanautata wanaendelea na uchunguzi kama  polisi wanahusika sheria itachukua mkondo wake.

Mwili wa marehemu Masanja umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Songea baada ya uchunguzi kukamilika watakabidhiwa na ndugu wa marehemu.

No comments:

Post a Comment