Monday 9 May 2016

Mfanyabiashara akamatwa kwa Kiwanda Bubu cha sukari.



MFANYABIASHARA mmoja Jijini Mbeya Bushir Sanga ,  amekamatwa akiwa na kiwanda bubu  cha kufungasha sukari
kwenye mifuko midogo yenye ujazo wa kati ya nusu kilo na kilo moja, ambayo ina nembo isiyokuwa ya Tanzania na kisha kuiuza mitaani na nyingine inadaiwa kusafirishwa nje ya nchi kinyemelea.
 mbeya
Ndivyo ilivyokuwa wakati wa zoezi hili ambalo limefanyika chini ya Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Mbeya, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa Sabi akiongozana na askari wa jeshi la polisi, wamefanya msako wa kushtukiza  na kuingia  mitaani kutekeleza agizo la rais Dk John Pombe Magufuli la kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha sukari.

Na ndipo akafanikiwa kubaini kiwanda bubu cha kufungasha sukari kinachodaiwa kufanya kazi hiyo kinyume cha sheria katika eneo la Soweto Jijini Mbeyakikiwa kwenye eneo la makazi ya watu.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akizungumza na wenyeviti wa Mitaa wa Jiji la Mbeya amewataka kuwafichua wafanyabiashara wote wakubwa, ambao wameficha sukari yao kwenye magodauni na kwamba kufanya hivyo ni kuhujumu uchum

No comments:

Post a Comment