Monday 9 May 2016

Tanzania,Zambia na China kukuza uwekezaji

Tanzania, Zambia pamoja na Jamhuri ya watu wa China zimeanza mazungumzo ya pamoja kwa lengo la kushirikiana kuimarisha sekta ya miundombinu hususan kufufua Reli inayounganisha Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kukuza biashara na uwekezaji.

Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi, amesema lengo ni kuangalia changamoto zilizopo, ikiwemo za kisheria na kiutawala katika shirika hilo ili hatimaye liweze kufanya kazi kwa namna iliyokusudiwa.

Awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2 za bidhaa kwa mwaka, wakati sasa inasafirisha tani laki 2 kwa safari inayotumia hadi siku kumi na mbili kutoka Dar es saalam hadi New Kapiri Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.
 Screen Shot 2016-05-09 at 4.23.30 PM
Balozi Kijazi amesema lengo ni kuifufua Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia, kwa kuangalia umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.

Awali Tanzania na Zambia zilikubaliana kuwekeza zaidi katika reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment