Saturday 22 February 2020

Msanii maarufu wa nyimbo za injili Rwanda anayedaiwa kujiua anazikwa leo

 Ibada ya wafu ikiendelea kwa ajili ya Bw. Kizito Mihigo ambaye alipatikana akiwa amekufa katika mahabusu ya polisi mjini Kigali
Msanii maarufu wa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo ambaye aliripotiwa kujiua katika mahabusu ya polisi nchini Rwanda anazikwa leo nchini Rwanda.
Mamia ya watu wamejitokeza kuusindikiza mwili wa Bw. Kizito Mihigo, akiwemo Bi Diane Rwigara, mwanasiasa wa upinzani na mfanyabiashara mjini Kigali.
 
Bw. Alifariki siku tatu baaada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Burundi, polisi wakimtuhumu kwa jaribio la kutaka kutoroka nchi na kujiunga na la waasi linalopigana dhidi ya serikali ya Rwanda.
Bw. Alifariki siku tatu baaada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Burundi, polisi wakimtuhumu kwa jaribio la kutaka kutoroka nchi na kujiunga na la waasi




Bw. Mihigo alipigwa marufuku kuondoka nchini Rwanda kutokana na mashitaka yaliyopita dhidi yake. 

Kifo cha Mihigo kiliibua hisia tofauti miongoni mwa wanyarwanda wanaoishi ndani na nje ya nchi huku wakitaka uchunguzi ufanyike kujua kilichosababisha kifo chake. 

Kizito mihigo alikua maarufu sana kwa nyimbo zake za injili zilizoikonga mioyo ya Wanyarwanda na Warundi wa ndani na nje ya nchi:

Mashirika ya kibinadamu pia yalitilia shaka kifo chake na kutaka uchunguzi huru ufanyike kuhusiana na kifo hicho. 

Hata hivyo Rwanda imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya kutaka uchunguzi huru kufanywa kuhusu kifo cha msanii maarufu wa muziki wa kiinjili Kizito Mihigo, ambaye alipatikana akiwa amefariki katika kituo cha polisi Jumatatu asubuhi.

Lakini baadhi ya watu wanaamini wimbo wake Igisobanuro cy'urupfu, ambayo tafsiri yake ni "maana ya kifo", aliyotoa mwaka 2014 siku kadhaa kabla ya kumbukumbu ya 20 ya mauaji ya kimbara ya Rwanda, ndio iliyomtia mashakani- kwa kugusia kile kinachodaiwa kuwa uhalifu uliofanywa na chama tawala cha Rwanda Patriotic Front.

Mihigo, ambaye alikuwa aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 mwaka 2015 kwa kupanda njama ya kupindua serikali, na kuachiliwa baadaye kwa msamaha wa rais Septemba 15 mwaka 2018 pamoja na wafungwa wengine zaidi ya 2,000

No comments:

Post a Comment