Saturday 22 February 2020

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 22.02.2020

 
Manchester United wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Wolves na Ureno Diogo Jota, 23. (Calciomercato) msimu ujao. 


Barcelona inajipanga kimsajili kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva, 25 dirisha la usajili litakapofunguliwa. (Daily Express)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson yuko tayari kusaini mkataba wake mpta kwasababu anaamini kwamba klabu inamaono mazuri hasa ya kipindi cha usajili.(Sky Sports)

Barcelona iko tayari kupambana na Chelsea katika kuwania usajili wa mlinda lango raia wa Cameroon, 23, anayechezea klabu ya Ajax, Andre Onana. (Diario Sport - in Spanish)

Aliyekuwa maneja wa Juventus na AC Milan, Massimiliano Allegri, amesema kwamba anataka kurejea katika kazini ifikapi Septemba huku Manchester United ikisemekana kuwa miongoni mwa vilabu vinavyomkodolea macho. (Daily Mirror)

 Lampard anasisitiza kwamba Chelsea ipitie tena uamuzi wake wa kumuweka pembeni mlinda lango anayelipwa mshahara wa juu zaidi mchezaji wa kimataia wa Hispania, Kepa Arrizabalaga, 25, (ESPN)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anafikiria kwamba Raheem Sterling, 25, wa Manchester City na Uingereza ni mshambuliaji mzuri lakini hayuko tayari kuzungumzia uwezekano wa kumsajili. (Goal.com)

Kocha wa Tottenham Mourinho ameweka wazi kwamba anajua watakaopangwa kuchezea Chelsea kwenye mechi dhidi ya timu yake katika ligi ya Premier League Jumamosi. (Daily Express)

Manchester City imemtafuta wakili ambaye amefanikiwa mara mbili kuzuia mchakato wa Uingereza kujiondoa Mungano wa Ulaya, kubatilisha uamuzi wa kupigwa marafuku ya kutocheza ligi ya mabigwa kwa miaka miwili. (Daily Mirror)

Arsenal wanapanga kumsajili beki wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah ambaye kwa mujibu wa mkataba wake anathamani ya pauni milioni 34. (Bild - in German)Klabu ya Inter Milan inajipanga

kutoa wachezaji kwenda klabu ya Verona kama sehemu ya mpango wa kumnasa beki wa Albania Marash Kumbulla, 20, ambaye pia anawaniwa na Liverpool. (Inside Futbol)

Beki wa Brazil David Luiz, 32, anaamini Arsenal wana kiwango cha ubora cha kuwafanya washinde Ligi ya Europa msimu huu baada ya kushindwa msimu uliopita. (Evening Standard)

Klabu ya Real Madrid wanamfuatilia kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17. (Marca)

Klabu ya Juventus imewaorodhesha mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus (22) pamoja na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Mauro Icardi (27) kama kipaumbele katika dirisha la usajili la mwishoni mwa msimu. (Tuttosport - in Italian)

No comments:

Post a Comment