Friday, 21 February 2020

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.02.2020


Wachezaji wa Atletico Madrid walishikwa na hasira na kushangazwa baada ya kukosolewa na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp. 


Atletico iliwafunga Liverpool 1-0 Jumanne katika raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Kombe la Mabingwa Ulaya, wachezaji wa Atletico wanamtaka Klopp kutizama mapungufu ya timu yake badala ya kuwakosoa. (ESPN)

Manchester City na Barcelona wanaminyana kumsajili beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, na klabu itakayofanikiwa kumnyakua itabidi itoe dau la zaidi ya pauni milioni 75. (Calciomercato)
Arsenal wanapanga kumsajili beki wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah ambaye kwa mujibu wa mkataba wake anathamani ya pauni milioni 34. (Bild - in German)

Beki wa pembeni wa Chelsea Marcos Alonso, 29, bado yungali anawaniwa na Inter Milan lakini klabu yake inatarajiwa kuongeza bei ya mauzo ya mchezaji huyo. (Calicomercato - in Italian)
Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish anaamini wataendelea kusalia na kocha Roy Hodgson baada ya kumpatia mkataba mpya. (Sky Sports



 Winga wa Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu anasema hana mpango wa kuihamisha familia yake kutoka kwenye nyumba yao jijini London. (Mail)

 Klabu ya Inter Milan inajipanga kutoa wachezaji kwenda klabu ya Verona kama sehemu ya mpango wa kumnasa beki wa Albania Marash Kumbulla, 20, ambaye pia anawaniwa na Liverpool. (Inside Futbol)



Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alikuwa akitaka kumsajili kiungo Christian Eriksen, 28, kabla raia huyo wa Denmark kuhamia Inter Milan akitokea Tottenham. (Manchester Evening News)

Klabu za Juventus na Inter Milan wanavutiwa kumsajili beki wa pembeni wa Chelsea Emerson Palmieri, 25, lakini bado ofa rasmi hazijatumwa ajenti wake abainisha. (Goal.com)


Beki wa Brazil David Luiz, 32, anaamini Arsenal wana kiwango cha ubora cha kuwafanya washinde Ligi ya Europa msimu huu baada ya kushindwa msimu uliopita. (Evening Standard)

Klabu ya Real Madrid wanamfuatilia kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17. (Marca)

No comments:

Post a Comment