Thursday, 12 May 2016

Bungeni Leo:Serikali kuunda sheria kudhibiti huduma za kifedha

Kutokana kuwepo kwa taasisi nyingi za kifedha ambazo nyingine hazifuati taratibu na kusumbua wananchi wanaohifadhi fedha serikali imesema inaandaa sera ya taifa ya huduma ndogo ya fedha ya mwaka 2016.
Akizungumza leo Bungeni Mjini wakati akifafanua serikali imechukua hatua gani juu ya utitiri wa taasisi za kifedha, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji amesema kuwa serikali inalitambua suala hilo na sasa wameanza kulichukulia hatua.

Mhe. Kijaji amesema kuwa serikali inazitambua taasisi ambazo zinawasumbua wananchi kwa kikiuka taratibu za kifedha jambo ambalo serikali imeamua kuchua hatua ya kuunda sheria hiyo itakayoweza kulishughulikia suala hilo moja kwa moja.

Aidha, Naibu Waziri huyo ameyataka mabenki pamoja na taasisi za kifedha, kutumia takwimu ili kuweza kujua taarifa halisi na historia za wakopaji pamoja ushindani uliopo ili waweze kushusha riba ambayo wananchi wengi wanaokopa katika mabenki wanalalamikia kuwa ni kubwa.

No comments:

Post a Comment