Thursday, 12 May 2016

Elimu bure changamoto kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakitoa burudani kwa kuimba wimbo wao maalum.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu nchini Tanzania, Bi. Catherine Sekwao, amesema kuwa watatumia maadhimisho ya wiki ya elimu duniani kutafuta utatuzi wa changamoto zinazowakabiliwa watoto wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Bi. Catherine, amesema kuwa watoto wenye mahitaji maalum nchini wengi wao wanakosa haki ya kupata elimu kutokana na kukosa miundondo mbinu wezeshi ya kuwafanya kupata elimu kama watoto wengine.

Mratibu huyo amesema mtandao huo umetaka kuwepo na mfumo wa elimu jumuishi ambao utawafanya watoto wenye ulemavu waweze kusoma shule za kawaida badala ya kuwatenga kwenye shule zao maalumu ili nao wapate elimu iliyobora na sawa na watoto wengine.

Bi. Catherine ameongeza kuwa hata sera ya elimu bure haikidhi mahitaji katika mfumo wa elimu jumuishi kutokana na ruzuku inayotolewa kwa kila mwanafunzi ambapo wakati mwanafunzi mwenye mahitaji maalum anamahitaji mengi zaidi kushinda mwanafunzi mwingine wa kawaida.

Kwa upande wake Mwalimu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Bi. Edith Ndosha, ameitaka serikali pamoja na wadau mbalimbali wawawezeshe watoto wenye ulemavu ambao wanakumbwa na changamoto nyingi katika upataji wao wa elimu.

No comments:

Post a Comment