SERIKALI imepiga marufuku kusafirisha wanyamahai wote nje ya nchi kwa miaka mitatu kuanzia leo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, bungeni mjini hapa jana wakati akifanya majumuisho ya hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2016/17.
“Kuanzia sasa (saa moja na dakika tano usiku) kwa miaka mitatu serikali imepiga marufuku usafirishaji wa wanyamahai wote kwenda nje ya nchi,” alitangaza Waziri Maghembe. Aliongeza kuwa, “Hata chawa za Tanzania hataruhusiwa kusafirishwa nje.
Na katika kipindi hiki cha miaka mitatu, idara ya wanyamapori itafanya kazi ya kuishauri serikali namna gani biashara hiyo itakavyoendeshwa”. Alisema watu wamekuwa wakisafirisha kila siku nje ya nchi wanyamahai ambao hawaruhusiwi kisheria na wanyamahai wengi hupelekwa Hong Kong, Thailand, Ulaya Mashariki na kwingineko duniani.
Profesa Maghembe alisema, “Hata wale tumbili waliokamatwa wanasafirishwa nje ya nchi bila ya vibali tuna jina chafu huko,” alisema. Waziri huyo alifafanua kuwa tumbili hao waliokamatwa wakipelekwa nje ya nchi kwa utafiti wa kibayolojia, watafiti wangelipwa mabilioni ya fedha wakati Tanzania ingelipwa dola 15 tu, ambayo ni sawa na bei ya tumbili mmoja
No comments:
Post a Comment