Friday 13 May 2016

Hii ndio Kauli ya Naibu waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla kuhusu Afya na Muungano.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amesema kwamba suala la huduma za afya siyo miongoni mwa mambo yaliyokubaliwa kushuhulikiwa na serikali ya Muungano.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma katika mkutano wa Bunge unaoendelea baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mwantum Haji (CCM) kutoka Zanzibar, kuitaka serikali kutoa misaada ya vifaa tiba na madawa kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Akijibu swali hilo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa afya si jambo la Muungano ila kuna ushirikiano na umoja wa hali ya juu kwa watendaji wa sekta ya afya hivyo.

Dkt. Kigwangalla ameelezea pia sababu za uongezeka kwa ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kubadilika kwa mtindo wa maisha pamoja na watu kutofanya mazoezi ya mwili ambapo ugonjwa huo huathiri figo, moyo, miguu na macho.

Aidha huduma za ugonjwa wa kisukari kwa sasa zinapatikana katika hospitali za wilaya ambapo serikali hadi sasa imetoa mafunzo kwa watumishi 150 wa zahanati mbalimbali ili waweze kutoa huduma hizo ili kukabiliana na wingi wa wagonjwa katika maeneo mbalimbali.

Pia Naibu Waziri ameahidi kuhakikisha huduma za afya katika hospitali za halmashauri nchini ili ziweze kuwahudumia wagonjwa wa kisukari.

No comments:

Post a Comment