Friday 13 May 2016

Yanga kurudiana na waangola tarehe hii.


Yanga wametamba kuwa hawataenda kinyonge au kwa upole kurudiana na wapinzani wao Sagrada Esperanca ya Angola kwa kuwa wanajua wapinzani wao watakuwa na nguvu kubwa hasa sababu wapo nyumbani.
Yanga itarudiana na Waangola hao Jumatano ijayo katika Kombe la Shirikisho baada ya awali kuwafunga mabao 2-0 jijini Dar.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wanakwenda wakiwa tayari wametuma mashushushu wawili waliokwenda kuandaa mazingira mazuri ya hoteli watakayofikia huko Angola.

Muro amesema mashushushu hao watasaidiana na mchezaji wao wa zamani wa timu hiyo, Said Maulid ambaye ni mwenyeji wao huko aliyekuwepo huko muda mrefu akiifundisha klabu moja ya Angola.

Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa kikosi chake na kudai kuwa kiko fiti kuelekea mchezo huo wa kimataifa.

Katika mechi ya kwanza mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva na Anthony Matheo aliyotokea benchi kuchukua nafasi ya Malimi Busungu. Kama ikisonga mbele Yanga itaingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment