Tuesday 17 May 2016

Hii ndio nafasi mpya ya Rooney katika Timu yake ya Taifa

 
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza, Alan Shearer amesema kuwa Wayne Rooney sio tena mshambuliaji namba moja katika timu yake ya taifa ya Uingereza.
Rooney ambaye anaongoza rekodi ya ufungaji wa muda wote ametajwa katika kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.

Shearer amesema Rooney  anafaa zaidi katika nafasi ya kiungo nyuma ya Harry Kane na Jamie Vardy.

Ameongeza kuwa ni lazima pawepo nafasi kwa ajili ya nahodha wa timu na amefurahi imepatikana.

Siku za Wayne Rooney kuwa mshambuliaji wa kwanza zimeisha.

Harry Kane na Jamie Vardy wanapaswa kuanza mbele lakini bado Rooney ana nafasi kubwa ya kucheza kama namba kumi kama kiungo wa kati, alisema Shearer.

Rooney ni miongoni mwa washambuliaji watano walioitwa katika kikosi cha Roy Hodgson siku ya Jumatatu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.

Wengine ni Harry Kane, Jamie Vardy, Daniel Sturridge na Marcus Rashford

No comments:

Post a Comment