Tuesday 17 May 2016

Watumishi wa wizara ya maliasili na utalii wametakiwa kufanya haya.

Watumishi wa wizara ya maliasili na utalii wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo visivyo vya uadilifu na
uzembe kazini kama kujishirikisha na biashara haramu ya nyara na magogo, ili kuepuka dhana ya utumbuaji majipu inayotekelezwa kwa sasa katika serikali ya awamu ya tano.

Kauli hiyo ilitolewa na katibu mkuu wa wizara hiyo,meja jenerali GAUDANCE MILANZI,alipokuwa anafungua mkutano wa baraza la 23 la wafanyakazi wa wizara ya maliasili na utalii inayofanyika katika ukumbi wa chuo cha utalii kilichopo jijini DAR ES SALAAM.

Amesema amatarajio yake ni kuwa wafanyakazi hao watatumia mkutano huo kujadili namna bora ya kuboresha utendaji kazi ili kulinda rasilimali za wanyamapori katika maeneo yote ili kuliletea taifa tija lakini endapo tu watafanyakazi kwa bidii na ufanisi ili kufikia malengo ya uanzishwaji wa mamlka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania(TAWA).

No comments:

Post a Comment