Saturday 10 September 2016

Zifahamu Dalili Saba kubwa za Mwanaume anazozionesha kwa Mwanamke anaempenda kwa Dhati.

Image result for husband material

Na H.Mshuka

Juzi mida ya saa tatu asubuhi nilikuwa katika kituo kimoja cha Daladala  nilikuwa nasubiri daladala  nilikuwa na  safari ya kutoka maeneo ya  Airport naelekea Kinondoni studio hapa hapa jijini Dar es salaam,kunashunghuli fulani za kikazi nilikuwa nakwenda kuzifanya .


Muda mfupi baadae daladala ilifika kituoni, idadi ya watu aikuwa kubwa kiasi cha kunipa nafasi ya mimi kuingia ndani ya daladala  nilipoingia katika daladala ile macho yangu yaliangaza huko na huko nikitafuta siti ya kukaa  nilifanikiwa kuiona  siti  moja ikiwa wazi  upande wa nyuma ya gari nami nikasonga moja kwa moja hadi katika ile siti na kukaa nakumbuka  pendeni kulikuwa na mama moja mtu mzima hivi aliyekuwa akiipapasa  simu yake ya kisasa (SmarPhone),nilipofika kanilimsalimu na  safari ikaendelea.

Tulipokuwa njia Deveva alifungulia  Radio ndani ya Daladala  ila sikumbuki vizuri ilikuwa  ni Radio gani ila kulikuwa na burudani za muziki zikiendelea nyimbo mbalimbali za Bongo Fleva  zilichezwa  moja baada ya nyingine baadae nikaisikia nyimbo ya Msanii wa mziki wa R'nB wa nchini Tanzania Benard Paul A.KA Ben Pol inayoitwa  Moyo Mashine ikiendelea kurindima ndani ya spika za  daladala ile  moja ya sehemu zilizonifanya nitabasamu ni ule ubeti wa pili uliokuwa unasema 

"Nafsi inanituma upendo uko nje ya maneno

Ila vitendo

Kama bubu akipenda atanena vipi kwa maneno

Pasina vitendo?
Kiziwi, hata ukimwambia “nakupenda” wata hasikii
Ila vitendo oh
Wewe sijui sababu za kukupenda
Siwezi sema, ila utaona ah"


Kilichonifanya nitabasamu ni huo ukweli mtupu ambao unapatikana  katika ubeti huo wa pili katika wimbo ya Moyo Mashine nilijiongeza kama wasemavyo vijana wa mjini na nikagundua kuwa ni kweli kuwa  wakati mwingine Vitendo vina nguvu zaidi kuliko maneno katika mambo mbalimbali  katika maisha. 

Nakumbuka pia baba yangu Mzee Mshuka aliwahi kuniambia kuwa "Mshindi niliyule anaetenda", akimaanisha kuwa  mtu yule anae  sema jambo au kutoa ahadi  na kuitekeleza kwa vitendo ndio Mshindi sahihi.


Katika Mahusiano pia  ukweli ubebwa na  vitendo ambavyo vinaonesha na kuwakilisha hisia za kweli zilizomo ndani ya moyo wa mtu  juu ya kitu fulani ambazo zinabebwa na  nakuelezewa na vitendo katika ile safari ya kuziwakilisha kwa mtu au kundi la watu waliokusudiwa.

Hata kwa  wanaume au wanawake katika mahusiano kuna muda wanapenda kuonesha vitendo zaidi kwa mtu yule ambae anampenda  na anataka kuishi nae katika maisha, pasipo kusema neno I LOVE YOU Au Nakupenda. 

zifuatazo ni tabia saba (7) kuu za mwanaume anazozionesha kwa mwanamke ambaye anania ya dhati ya kutaka kuishi nae katika maisha. 

1. Anakupigia simu mara kwa mara au kukutumia ujumbe na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.
  
2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu.
  
3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake, Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume.
  
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!
  
5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.
  
6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda.
  
7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.
 
Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka atengeneze future pamoja na wewe. 



USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment