Mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza leo wamesitisha shuguli zao kwa muda baada ya mtu mmoja kuzua taharuki kwa kunusurika na kifo, baada ya kujirusha kutoka juu ya mnara wa moja ya Kampuni ya simu za mkononi hadi ardhini.
Si mwingine ni kijana Musa Shaaban jina linalomtambulisha, baada ya kupanda juu ya mnara huo na kisha kuanza kuvuruga miundombinu ya Mawasiliano ya Kampuni hiyo, tukio lililovuta hisia za wengi, huku baadhi yao wakiingiwa na hofu ya kukosa Mawasiliano.
Kutokana na hofu hiyo kikosi cha uokoaji cha zima moto wakishirikiana na askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza wakapanda juu ya mnara huo, ili kunusuru uhai wa kijana huyo na miundombinu ya Mawasiliano, lakini cha ajabu kijana huyo akajirusha.
Jitihada za kumnurusu na kifo kijana huyo zilipokamilika, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza likalazimika kumchukua na kisha kumkimbiza Hopitali, ambapo hadi wakati huu amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure.
No comments:
Post a Comment