Waziri mkuu Kassimu Majaliwa amewataka wakazi wa dar es salaam hususan wanaotumia mabasi yaendayo haraka kuhakikisha wanatumia huduma hiyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa ikiwemo suala la ukataji tiketi pamoja na matumizi yake ili mradi huo uweze kuwa endelevu na wenye tija kwa wananchi na taifa.
Waziri Mkuu amebainisha kuwa serikali imedhamiria kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi hivyo changamoto ndogondogo zinazoibuka zitaendelea kutatuliwa ikiwemo kuboresha mfumo wa ukataji tiketi ambao umekuwa ukilalamikiwa na kusababisha msongamano vituoni
Aidha amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha watu madaraja ya kuvukia abiria hayageuzwi mahala pa kulala kama ilivyojitokeza.
Mapema alipotembelea mradi huo wa mabasi yaendayo haraka, Waziri Mkuu alipanda basi kutoka kivukoni hadi Kimara akiambatana na aliyekuwa mwenyekiti wa mamlaka ya usafirishaji dar David Mwaibula ili kutathmini mwenendo wa mabasi hayo ambapo ametumia dakika 55 katika safari hiyo na kubaini baadhi ya changamoto zinazochangia mabasi hayo kuchelewa katika baadhi ya makutano ya barabara ambapo amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo kitafungwa kifaa maalumu kwenye makutano hayo ambacho kitatoa ishara kwa magari mengine ili kuruhusu mabasi hayo kupita.
No comments:
Post a Comment