Wednesday, 18 May 2016

Hili ndio jipu lililoiva lililotaja Mh.James mbatia.

Mbunge wa Vunjo na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano James Mbatia amesema kivuko cha Dar es salaam kwenda Bagamoyo ni jipu lililoiva kutokana na ripoti kuonyesha ni kivuko feki na kibovu.
Mbatia ameyasema hayo Bungeni wakati akitoa mchango wa kambi ya upinzani kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

''Kivuko cha Dar es salaam kwenda Bagamoyo ni jipu ambalo limeiva kwa viwango vyote vya sasa na linatakiwa litumbuliwe mara moja ni dhahiri kuwa kivuko hicho kilichonunuliwa na TEMESA chini ya uongozi wa Waziri wa Ujenzi wa serikali ya awamu ya nne ambaye sasa ndiye Rais wetu wa sasa wa Tanzania ripoti za CAG zinaonyesha ununuzi wa boti hiyo feki na mbovu uligharibu zaidi ya shilingi bilioni 7.9''- Amesema Mbatia.

Aidha Mbatia ameitaka serikali ya awamu ya tano kuweka mifumo endelevu inayojali na kukuza utu wa mama Tanzania na kuachana na mfumo wa kutumikia mfumo ambayo ni dhambi kwa taifa.
Aidha Wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa shilingi 4,895,279,317,500.00/= ili kutekeleza majukumu yake ya kuboresha sekta za ujenzi , uchukuzi na mawasiliano nchini.

No comments:

Post a Comment