Sunday, 15 May 2016

Kauli ya Naibu waziri ofisi ya rais TAMISEMI Seleman Jaffo kwa watanzania kuhusu Mabasi yaendayo kasi.

 
Naibu waziri ofisi ya rais – TAMISEMI Seleman Jaffo amewataka wananchi kutunza miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka – DART pamoja na mabasi yenyewe ili kuufanya mradi huo wa kipekee katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kuwa endelevu.


Naibu Waziri huyo amesema Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zenye maendeleo makubwa baada ya kukamilisha miradi mikubwa iliyo kwenye mpango ya utekelezwaji, ukiwemo ujenzi wa barabara za juu fly over kwenye makutano ya barabara za Nyerere na Manderl ambako harakati za ujenzi zimeanza lakini pia awamu ya pili ya mradi wa DART utakaohamia barabara ya Kilwa itakayowaunganisha wakazi wa Mbagala kabla ya mradi wa tatu utakaowahusu wakazi wa Gongo la mboto.

Alikuwa akizungumza katika ziara ya kutembelea mabasi yaendayo haraka yanayotarajia kuanza kutoza nauli kesho ambapo amewataka watendaji wa DART kuharakisha mfumo wa ulipaji wa nauli kwa kutumia kadi ili kuepuka upotevu wa mapato unaoweza kusababishwa na watu wasio waaminifu huku akiliagiza jeshi la polisi kuimarisha ulinzi kwanzia vituoni.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa UDART David Mgwassa amesema huduma ya mabasi hayo itaanza saa 11:00 alfajili hadi saa 6:00 usiku kwa kutumia mfumo wa tiketi ambazo zitapatikana katika kila kituo huku wakiendelea kukamilisha mfumo wa kadi uanaotarajiwa kuanza kutumika rasmi baada ya siku tano.

No comments:

Post a Comment