Sunday, 15 May 2016

Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda akutana na Wauza nyama machinjio ya Vingunguti na kuzungumza haya.

 
Wafanyabiashara wadogo, wauza nyama katika machinjio ya Vingunguti jijini dsm leo wamekutana na mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda.

Naibu Meya wa manispaa ya Ilala  pamoja na wawakilishi wa benki ya wananchi dsm-DCB kuelezea changamoto mbali mbali ikiwemo ucheleweshwaji wa mikopo ya kibiashara lakini pia hali mbaya ya kiuchumi baada ya machinjio ya Vingunguti kufungwa kutokana na Uchafu.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao Naibu meya wa Ilala amesema Halmashauri ya manispaa ya Ilala kupitia mapato yake imetenga asilimia kumi kwa ajili ya Vijana wajasiriamani ambapo tayarri zimetolewa lakini utaratibu wa sasa wa fedha zote za halmashauri kupelekwa benki kuu na baadae kuingizwa DCB ili ziwafikie wananchi inasababisha mikopo hiyo kuchelewa.

Mkuu wa mkoa wa dsm ameahidi kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha fedha hizo zinatoka kwa wakati ili wananchi wazipate ambapo pia ameahidi kuwasaidia katika kuwashawishi watoa huduma za kifedha kuweka matawi katika machinjio hayo ili kupunguza hatari ya kutembea na fedha wakati wa kununua au kuuza mifugo au nyama katika machinjio hayo.

Aidha Bw,Makonda alitembelea na kufanya Ukaguzi katika machinjio hayo kuangalia ukarabati uliofanyika na kusema kuwa hivi sasa hali ya miundombinu imeboreshwa maradufu ili kulinda afya za walaji.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa dsm amewataka wakazi wa dsm kujitokeza kesho katika mapokezi ya mwenge wa Uhuru unaotokea Zanzibar ambapo utakuwa jijini kwa ziara ya siku tatu itakayoanzia wilaya ya kinondoni na kuzindua miradi saba ya maendeleo

No comments:

Post a Comment