Sunday, 15 May 2016

TANESCO inawataka watu hawa kujisalimisha kabla hawajatumbuliwa.

 Screen Shot 2016-05-15 at 4.16.59 PM
Shirika la umeme Tanzania TANESCO limewatahadharisha wamiliki wa mabango ya matangazo yanayotumia umeme bila kulipia kujisalimisha wenyewe katika ofisi za shirika hilo kabla sheria haijafuata mkondo wake.


Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na mkaguzi mkuu wa mita kanda ya Dar es salaam na Pwani Mrisho Sangiwa akiwa kwenye oparesheni maalumu ya kukagua mabango hayo ambayo ameitaja kuwa ni endelevu amesema oparesheni hiyo inaenda sambamba na ukaguzi wa taa za barabarani.

Sangiwa amesema yapo baadhi ya mabango yemeunganisha umeme moja kwa moja kutoka kwenye ngunzo na wengine wamechezea mita, hivyo wamiliki wa mabango wanaohisi mita zao hazisomi inavyotakiwa ama zimechezewa kwa lengo la kutumia umeme bila kulipia watoe taarifa katika ofisi za TANESCO kwani endapo watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kulipa faini na kufikishwa mahakamani

No comments:

Post a Comment