Baadhi ya wazalishaji wa sukari nchini wamepongeza juhudi za Rais Dk JOHN MAGUFULI za kudhibiti uingizaji holela wa sukari toka nje ya nchi hatua ambayo itanusuru viwanda vilivyopo pamoja na kuongeza idadi ya viwanda katika siku za usoni.
Meneja uendeshaji wa Superdoll kampuni inayomiliki kiwanda cha sukari cha KAGERA , ABEL MAGESE amesema hatua ya Rais ya kutaka kuimarisha viwanda hapa nchini haina budi kuungwa mkono.
Meneja huyo uendeshaji wa SUPERDOLL amesema suala la sukari linahujumiwa na baadhi ya wafanyabiashara nchini ambao wanafaidika na uingizaji holela wa sukari unaokwamisha wazalishaji wa ndani kufanya biashara yenye tija.
Hata hivyo akizungumzia uhaba wa bidhaa hiyo, katika soko la ndani kwa sasa Bwana MAGESE amesema kimsingi sukari ipo ingawa amekiri kwamba kuna sehemu bei yake imekuwa juu ingawa hali hiyo haitarajiwi kuendelea kwa kipindi kirefu kwa vile viwanda vya sukari vya ndani kikiwemo Kagera sugar vinatarajiwa kuanza uzalishaji siku chache zijazo baada ya kusitisha uzalishaji kutokana na msimu na ukarabati wa mashine
No comments:
Post a Comment