Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Paul Mkonda
wamegundua Sukari iliyofichwa katika jengo la ghorofa tisa ambalo liko katika jengo linalojengwa lililopo katika eneo la Hananasifu -Kinondoni huku mmiliki wa sukari hiyo Bw,Bashir Ismail mwenye asili ya kiasia akitiwa mbaroni na jeshi la Polisi
Sukari hilo inadaiwa kuingizwa usiku katika jengo hilo huku kikiwa katika mifuko ya viroba vya kilo 25,na ishiri lakini pia ikifungwa katika mifuko midogo ya Plastiki ya kilo moja moja.
Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari amesema baadhi ya wafanyabiashara wameendelea kukaidi agizo la serikali kwa kuficha sukari katika maghara na maeneo mbali mbali na kuahidi kuwa Oeresheni dhidi ya wafanyabiashara hao ni ya kudumu.
Bw, Bashir Ismail ambaye alikuwa chini ya Ulinzi wa jeshi la Polisi alihojiwa na kudai sukari hiyo iliyohifadhiwa katika jengo hilo inapelekwa katika vituo vya kijamii ingawa alishindwa kujieleza jinsi mazingira iliyowekwa huku ikifanyika kazi ya kuweka katika viroba kwa kuwa eneo hilo linafanyika ujenzi na sio kiwandani.
Aidha Mkuu wa mkoa amewaonya wafanyabiashara wa Mkoa wa dsm kuwa wamebaini kuwapo njama za kuficha bidhaa nyingine ikiwemo mchele na mafuta katika kipindi hiki kuelekea mfungo wa ramadhani na kutoa onyo lifuatalo.

No comments:
Post a Comment