Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku
Galawa, amewaagiza Maafisa Tarafa kushiriki katika zoezi la uhakiki wa
watumishi katika halmashauri za mkoani humo ili kuwezesha shughuli hiyo
kuwa na tija zaidi.
Katika
kikao chake na maafisa hao,Galawa amewaagiza maafisa hao kuwa na majina
na idadi ya watumishi wote waliopo katika maeneo yao ili kuwezesha
utunzaji mzuri wa rekodi za watumishi.
Wakati huo huo Galawa ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kuleta orodha ya watumishi wote wakiwamo waliopo masomoni ambapo taarifa zao zinapaswa kuonesha walianza lini masomo na wanataraji kumaliza lini.
Amesema taarifa hizo zitaiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za watumishi waliopo sambamba na sifa za kitaaluma sambamba na mapungufu yaliyopo katika kada tofauti za utumishi wa umma.

No comments:
Post a Comment