Serikali imeingiza sukari tani elfu 11957 ambayo imeingia jana jioni ambayo itasambazwa katika kanda zote hapa nchini ili
kukabiliana na uhaba wa sukari uliopo ambao umeibuka baada ya kubainika wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo na kusababisha wananchi kuuziwa kwa bei ya juu na wengine kushindwa kumudu gharama hizo.
waziri mkuu Kassim Majaliwa |
Anaungana na rais DK.John Pombe Magufuli kuwahimiza wafanyabiashara walioficha sukari kutoa bidhaa hiyo ili wananchi waweze kuitumia kama walivyokubaliana hivyo ametumia fursa hiyi kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo lakini pia serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari linaodoka kabisa baada ya kuongeza uzalishaji wake.
Katika hatua nyingine waziri mkuu kassim Majaliwa amezungumzia mkutano mkubwa utakaowakutanisha viongozi 60 duniani wenye lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na suala rushwa ambapo kwa Afrika ni Tanzania na Nigeria ndio zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi hizo 60 ambapo Waziri mkuu atamwakilisha rais katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment