Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa Takukuru imempa masaa 36 mmiliki wa kampuni ya AL NAEEM Enterprises awe
ameshatoa tani 1800 za sukari ambao ziko katika bandari ya Dar es salaam ili zisambazwe katika masoko nchini
Mapema leo taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru wametembelea katika bandari ya Dar es salaam kwa lengo la kujionea kontena za sukari zilizokuwa zimehifadhiwa bandarini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuthibitisha uwepo wa kontena hizo kaimu mkurugenzi wa uchunguzi Pccb Leonald Mtalai amesema walipata taarifa za uwepo wa kontena hizo bandarini hapo ambapo miliki wake hakutaka kuzitoa kwaajili ya kuzisambaza sokoni
Licha ya kuamuliwa mmiliki huyo kuisambaza bidhaa hiyo ndani ya masaa 36 bado kulikuwa na mkanganyiko wa maelezo ya uingia wa tani hizo za sukari kati ya mmiliki na Ticks ambapo mmiliki amedai kuwa sukari hiyo imeingia ndani ya miezi mitatu huku tics ikidai ameipokea makontena hayo zaidi ya miezi mitano iliyopita .
Awali ilielezwa kwamba tani hizo 1800 za sukari zilikuwa zinapelekwa nchini Burudi ila kutokana na hali ya machafuko inayoendelea nchini humo ikabidi mmiliki huyo azisambaze hapa nchini
No comments:
Post a Comment