Sunday, 22 May 2016

Manchester United washinda Kombe la FA,Mourinho aonekana uwanjani.

Red Devils captain Wayne Rooney poses with the FA Cup after Saturday's 2-1 victory over the Eagles  
Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezewa uwanja wa Wembley.

Ni mara yao ya kwanza kushinda kikombe hicho tangu 2004.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata na Jesse Lingard.
Bao la kufutia machozi la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon.
Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofana kwa klabu hiyo.
Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Current United boss Louis van Gaal insists he has nothing to prove after winning the FA Cup 
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.
"Ni muhimu sana kushindia klabu kikombe hiki, kwaa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya hivyo," amesema
 Former Chelsea manager Jose Mourinho has been earmarked to take over at Manchester United
Jose Mourinho akitazama mechi

No comments:

Post a Comment