Meneja Uhusiano Mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. William Gatambi. |
Wakala wa mabasi yaendayo kwa haraka nchini
Tanzania -UDART imesema kuwa suala la watumishi wa umma wakiwemo walimu
na polisi kupanda bure katika mabasi hayo bado halijafanyiwa utaratibu
hivyo wataendelea kulipa kama watu wengine.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam, jana Meneja Uhusiano wakala wa mabasi yaendayo
haraka UDART, William Gatambi, amesema endapo watafanya hivyo italeta
mchanganyiko kwa sababu mfumo uliopo hauruhusu mtu kupita bila kulipia.
Bw. Gatambi amesema kwa sasa wanatumia mfumo wa karatasi wakati wakiwa kwenye mchakato wa kuandaa mfumo wa tiketi za kieletroniki ambao wanaweza kufanya utaratibu ambao unaweza ukatoa nafasi kwa watumishi hao kupanda bure.
Aidha, Afisa Uhusiano huyo amesema katika kukabiliana na changamoto za foleni katika vituo hivyo wameamua kuzikata tikeki kabisa ili kusiwe na usumbufu kwa wasafiri wanaowahi kufika vituoni kwa sababu mara nyingine mtandao wa kutoa risiti unafanya taratibu katika utoaji risiti.
Aidha, amesema kuwa abairia hawana haja ya kukimbiala mabasi hayo hata kama limejaa kwa kuwa kupishana kwake yanachukua muda mfupi kituo kwa kituo hivyo ni vyema mtu kusubiri baada ya kuona gari limejaa.

No comments:
Post a Comment