Thursday, 19 May 2016

Mbowe azungumza haya kuhusu uvunjifu wa sheria za utawala.

Mbunge wa Jimbo la Hai ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe ameliambia Bunge kwamba kuna mwingiliano wa utendaji na uvunjaji wa sheria katika halmashauri na manispaa zinazoongozwa na upinzani nchini.
Mbowe ameyasema hayo Bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza katika wizara ya TAMISEMI ambapo ameitaka serikali kutoa kauli kuhusu halmashauri na manispaa ambazo zinaongozwa na viongozi wa upinzani kuheshimiwa na kupewa nafasi ya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu na kuepuka migongano isiyo na ulazima.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amesema kwamba kinachotakiwa kufanyika ni kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kuzingatia taratibu za kiutawala.

Aidha Jafo amesisitiza kuwa Mkuu wa Wilaya hawezi kuona mambo yakiaribika huku akiacha kuchukua hatua kwa kigezo cha eneo hilo kuongozwa na upinzani kwani ilani inayotekelezwa kwa sasa ni ya chama tawala hivyo kama jambo lina maslahi kwa taifa ni lazima litaingiliwa kati ili kupata ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment