Friday 13 May 2016

Msafara wa Rais Dr.Magufuri wasababisha wamachinga kutawanywa kwa mabomu ya machozi kwa namna hii jijin Dar es salaaam.


Wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga kutoka maeneo ya kariakoo jijini dsm leo wamejikuta wakitawanywa na mabomu ya machozi pamoja na baadhi yao kutiwa mbaroni baada ya kutaka kuzuia msafara wa Rais Dr.Magufuri akitokea airpoti kuwasilisha malalamiko yao ya kuondolewa katikati ya jiji na kupelekwa katika maeneo waliyopangiwa.


Wafanyabiashara hao wamedai kuwa maeneo waliyotakiwa kwenda sio rafiki kibiashara na huku wakidai kuwa zoezi linaloendelea la kuwaondoa ni uonevu na kutaka watafutiwe eneo katikati ya jiji kama ilivyopendekezwa ikiwemo kufungwa baadhi ya barabara ili wafanye biashara.

Mkusanyiko huo wa wafanyabiashara katika eneo hilo ulianza kusambaratika kidogo kidogo huku wakijigawa katika makundi hali iliyosabaisha jeshi la Polisi kikosi cha FFU kujipanga na kuanza kuwatawanya.

halmashauri ya manispaa ya ilala ilitoa mpaka ijumaa ya leo kuwa wafanyabiashara wote wa kariakoo wanatakiwa kwenda katika maeneo waliyooelekezwa ili kupunguza msongamano katikati ya maeneo ya kariakoo

No comments:

Post a Comment