Friday 13 May 2016

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi atoa kauli hii kuhusu Serikali ya Rais Dk. Magufuli.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Injinia Edwin Ngonyani amesema kwamba serikali ya awamu ya tano ikisema jambo inamaanisha na ikiahidi inatenda kama ilivyo ahidi hivyo wananchi waiamini.
Ngonyani ameyasema hayo Bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge Juma Nkamia (CCM) kuhusu kipande cha barabara kutoka chuo cha Mipango Dodoma kwenda Msalato kiasi cha kilomota 8 na zaidi ziliahidiwa kujengwa kwa lami na hadi sasa bado hazijafanyiwa kazi.

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Ujenzi Ngonyani amesema serikali hii ikiahidi inatenda na kwamba barabara hilo tayari mkandarasi atawasili katika eneo la kazi baada ya kulipwa stahiki zake.

Aidha serikali imeitaka TANROADS kuanza kukarabati barabara mbalimbali nchini ambazo zimeharibika kufuatia mvua za masika kunyesha

No comments:

Post a Comment