Tuesday 3 May 2016

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yafanyika jijini mwanza leo

linus

Leo ni siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo hapa nchini maadhimisho ya kitaifa yanafanyika Jijini Mwanza. Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye, ni miongoni mwa walioakwa kwenye maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi ni Jaji Mkuu wa Tanzania Othman Chande.

Kabla ya kilele cha maadhimisho hayo leo, wadau wa sekta ya habari nchini walikutana kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo, ikiwemo kuminywa Uhuru wa utoaji wa taarifa, Maslahi duni ya waandishi wa habari, kukosekana kwa mikataba ya kazi pamoja na baadhi ya sheria kandamizi.

Katika majadiliano hayo, wadau hao wamekuwa na mitazamo inayolenga kuboresha sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na mamlaka za usimamizi na utawala kuhakikisha zinajenga mazingira rafiki ya kuwawezesha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment