Thursday 5 May 2016

Tazama Full Time ya matokeo ya Real madrid VS Manchester City hapa(+picha)

Real Madrid vs Man City LIVE score: UEFA Champions League 2016
Manchester City wameshindwa kufika katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo
uliokua wa kuvutia tena wa aina yake ulio malizika kwa man city kufungwa goli  1-0.
 
Baada ya kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.

Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo.

 Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao 4,500.
Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. 
 

  • Real Madrid:
  •  Navas, Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo, Modric, Kroos, Isco (James Rodriguez), Bale, Jese (Lucas Vazquez), Ronaldo
  • Real Madrid subs: Casilla, Varane, Danilo, Kovacic, Mayoral


  • Manchester City starting
  •  Hart, Sagna, Kompany, Otamendi, Clichy, Fernando, Fernandinho, Toure (Sterling), Navas (Iheanacho), De Bruyne, Aguero

  • Man City subs: Caballero, Kolarov, Mangala, Delph, Bony








  • Real sasa watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza





    Real Mandrid akiwasili katika uwanja wao wanyumbani Bernabeu kabla ya mechi

    No comments:

    Post a Comment