Agizo la Rais Dk John Pombe Magufuli la kuwataka wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapofanya mauzo limeshindwa kutekelezeka kwa baadhi ya vituo vya mafuta vya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Channel ten imetembelea vituo mbalimbali vya mafuta mjii hapa na kushuhudia baadhi ya vituo vikifanya biashara kutwa nzima bila kutoa risiti kituo cha Kisumapai kilichopo katikati ya mji hapo hapakuwa na kitabu cha risiti wala mashine ya EFD mmiliki wa kituo hicho Hinju Ngonyani alikataa kurekodiwa hata hivyo amekili kuwa hawatoi risiti kwa sababu wateja wao hawadai risiti anayehitaji anakatiwa risiti ya mashine inayotumika duka la spea za magari.
Kitendo cha kutotoa risiti licha ya kuikosesha serikali mapato baadhi ya watu wamejiwekea utaratibu wa kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha kama alivyokutwa mmoja akilalamikia tabia ya kutooa risiti.
Katika kituo cha Mdaula channel ten ilikutaa mashine ya EFD ya kutolea risiti changamoto iliyopo ni kwa wafanyakazi hawana uelewa wa kutoha juu ya kuzitumia hivyo wameiomba mamlaka ya mapato TRA mkoani hapa kuwapatia elimu ya matumizi ya mashine hizo.
Kamera ya Channel ten ilifika ofisi za mamlaka ya mapato mkoani hapa kupata ufafanuzi wa baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na madhara ya kutotoa risiti kaimu meneja Lamson Tulyanje amesema kuwa mapato wanayategemea kutokana na utoaji wa risiti hivyo wafanyabiashara wasipotoa risiti wanaiibia serikali.
Kodi ni uhai wa taifa mapato ya serikali hutokana na makusanyo ya kodi huwezi kutoza kodi bila kujua kiwango cha biashara kilichofanywa bila risiti ni vigumu kujua kodi sahihi inayopaswa kulipwa kulipa kodi ni uzalendo Geofrey Nilahi chnnel ten Songea
No comments:
Post a Comment