Wednesday 4 May 2016

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli huu hapa

 

Asha Migiro ateuliwa na Rais Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza

                           JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                      KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
04 Mei, 2016


No comments:

Post a Comment