Monday 16 May 2016

Waziri Mkuu ajibu haya kuhusu suala la bunge kutooneshwa "LIVE".


 
Akijibu swali kuwa ana maoni gani juu ya Bunge kutorushwa ‘live’, Majaliwa alisema, hatua hiyo ilichukuliwa ili kuwawezesha watu kufanya kazi kama ambavyo kaulimbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu inavyosema.

“Bunge la Tanzania lilikuwa ni pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani ambalo lilikuwa likirushwa moja kwa moja kuanzia asubuhi hadi usiku. Ina maana katika kipindi cha Bunge la bajeti, ambalo linaendeshwa kila siku kwa miezi mitatu, Watanzania nao wangekuwa ‘Live’ kwa miezi mitatu,” alisema.

Alisema, walilazimika kujifunza kutoka kwenye mabunge mengine. “Hivi hapa Uingereza mnaangalia Bunge ‘live’ kila siku?” Alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa kuwa linarushwa kwa kipindi kisichozidi dakika 15 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu pekee.

Akitoa ufafanuzi, aliwaeleza kuwa Bunge la Tanzania linarusha ‘live’ kila siku asubuhi wakati wa maswali ya kawaida na Alhamisi asubuhi wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu, lakini mijadala yote hurekodiwa na kuhaririwa na kisha kurushwa kuanzia saa 8:00 hadi saa-9:00 mchana na saa 3:00 hadi saa 4:00 usiku kwa siku husika.


No comments:

Post a Comment