Monday 16 May 2016

Waziri Mahiga azungumza haya kuhusu suala la Rushwa nchini kwa kauli hii.

 
 Dk Augustine Mahiga alisema, kuitishwa kwa mkutano wa kupambana na rushwa nchini Uingereza ni moja ya jitihada za Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi ya rushwa.


“Kukosekana kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya, biashara ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi ya mambo yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana mahali pa kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili tatizo hili,” alisema Balozi Mahiga.

Alisema rushwa ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David Cameron ameamua kuanzisha jambo hilo kutafuta njia za kukabili janga hilo kubwa.

“Sote tunatambua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii ‘movement’ lakini ni faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na hii ni kwa sababu ya uongozi na ujasiri wa Rais Dk John Magufuli ambaye kwa kweli ni ‘game changer’ (akimaanisha kuwa amebadili mwelekeo wa Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea maovu,” alisema huku akishagiliwa.

Mkurugenzi Mkuu Takukuru Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alisema, vita ya rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia mwito alioutoa Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20, 2015.

Alisema wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda nayo hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha tabia na utamaduni uliojikita kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment