Tuesday 31 May 2016

Waziri mkuu Majaliwa aeleza mpango huu wa serikali kuhusu utunzaji vivutio vya utalii nchini.

Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amesema serikali inaendelea na mikakati ya  kutoa elimu kwenye maeneo yote yenye vivutio vya  urithi  vya asili na kiutamaduni zikiwemo hifadhi  lakini pia inatarajia  kutengeneza sheria zitakazodhibiti maeneo haya na wingiliano na shughuli za kibinadamu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anafungua  mkutano wa kimataifa wa siku nne unaohusu kulinda urithi wa dunia Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu unaofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha AICC ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la UNESCO na kushirikisha wadau na wataalamu mbalimbali katika Nyanja za uhifadhi na urithi wa dunia na mandeleo endelevu.

Waziri mkuu amesema jitihada za pamoja zinahitajika kwa kila mtanzania kwa kushirikiana na serikali zaidi akisisitiza wananchi wanaoishi kwenye mzunguko wa maeneo hayo kuwa mstari wa mbele kuyatunza ,kuyalinda na kuyahifadhi badala ya kuendelea kukinzana na serikali inapoweka mikakati ya kulinda maeneo hayo.

Waziri wa maliasili na utalii Jumanne Mghembe amesema wizara yake imejipanga vyema kuhakikisha inalinda na kutunza vivutio vyote vya utalii vilivyopo nchini huku mwakilishi wa mkurugenzi wa shirika la kimataifa la UNESCO Dakta Mechtild Rosseler amesema ni matarajio yao kuwa mkutano huo utakuwa na  manufaa makubwa na maapendekezo yatapelekwa kwa nchi wananchama wa mkataba wa unesco wa mwaka 1972,wahisani wa kimaendeleo wenye viwanda na jumuiya za kiraia na kwa jamii ili kuweza kuyatekeleza.

Tanzania inapewa heshima hii ikiwa ni moja ya nchi tajiri kwa urithi mbalimbali wa utamaduni na asili yakiwemo maeneo saba kati ya tisini na moja yaliyowasilishwa kwenye orodha yaUNESCO  ya urithi wa dunia

No comments:

Post a Comment