Wednesday 1 June 2016

Hivi ndio Polisi walivyofanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu kutoka Ethiopia hii leo.

Wahamiaji haramu 71 kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa katika eneo la kigamboni jijini dsm baada ya kuingia nchini wakitokea mombasa nchini kenya kwa njia ya bahari na baadae kusafirishwa kwa njia ya barabara kuelekea nchini afrika kusini.

Kutiwa mbaroni kwa wahamiaji hao kunatokana na taarifa za raia wema kutoa taarifa polisi baada ya kuona Lori aina ya Scania lenye namba T 246 BBG likielekea katika Ufukwe wa bahari eneo maarufu la kuingiza mali za magendo ambapo baada ya polisi kufika walifanikiwa kuwatia mbaroni dereva wa gari hilo,utingo pamoja na wakala wa wahamiaji hao haramu.

Hata hivyo baada ya kuingizwa katika gari kuelekea kituo cha polisi katika hali ya kutatanisha Mtuhumiwa namba moja aliyekuwa akiwasafirisha wahamiaji hao hakuonekana baada ya kudaiwa kushushwa njiani na askari waliomkamata hali iliyoashiria mtuhumiwa kutoa rushwa na huyu hapa dereva wa gari hilo anaeleza.

Akisimulia Mkasa huo dereva na utingo ambao ni wakazi wa mbeya walisema walikodiwa baada ya kushusha mzigo wa ndizi katika soko la ndizi manzese,na baadae wakaelezwa kuna mzigo

No comments:

Post a Comment