Wednesday 1 June 2016

Hivi ndio mama mjamzito anavyo wezakuthirika kutokana na kutoenda katika Vituo vya huduma ya Afya..

Idadi kubwa ya baadhi ya akina mama wajawazito mkoani Kigoma, inadaiwa hawana utamaduni wa kwenda kwenye vituo vya huduma ya afya wakati wa ujauzito na hivyo kuhatarisha afya ya mama na mtoto.


Miongoni mwa sababu ambazo zimeelezwa kuwa zinachangia kushusha idadi ya akina mama kwenda kwenye vituo vya afya mkoani Kigoma, ni kutokana na Umbali mrefu wa vituo vya afya pamoja na fikra potofu za akina mama hao.

Ili kuleta hamasa ya akina mama kuhudhuria kwenye vituo vya afya mkoani Kigoma, Taasisi ya World Lung imezundua kampeni ya redio inayolenga kuongeza idadi ya wanawake wanaojifungua katika vituo vya huduma za afya, ikilenga kuwahimiza akina mama kutafuta tiba mapema wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua.

Kampeni hiyo ya miezi mitatu itakayogharimu zaidi ya shilingi milion 160 iliyopewa jina la THAMINI UHAI, imelenga kuongeza ufahamu kuhusu dalili hatarishi, wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua.

Tanzania inakadiriwa kuwa ya nne katika bara la Afrika na ya sita duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya uzazi. Takwimu zinaonyesha kuwa Akina mama 398 kati ya laki moja wanaojifungua hufariki dunia kutokana na matatizo ya uzazi.

No comments:

Post a Comment