Monday, 5 February 2018

Usiyoyafahamu kuhusu Kingunge Ngombale Mwiru.

Image result for kingunge ngombale mwiru

Nguli wa siasa Tanzania na Afrika Kaitano Ngombale Mwiru alijipa jina la kingunge lenye maana ya kitu au kisiki kikubwa,kigumu, madhubuti imara kisichoyumba .


Asili ya neno Kingunge ni kilwa mkoani Lindi kwa wenyeji wa kabila la Matumbi.

Kingunge alifariki dunia usiku wa kuamkia Februari 2 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kung’atwa na mbwa akiwa nyumbani kwake kijitonyama Dar es salaam
Kwa mujibu wa Enock Ngombale kaka yake alijiita Kingunge baada ya kurudi kutoka masomoni nje ya nchi alikokuwa kwa zaidi ya miaka 10 na aliporudi  alikuja na msimamo wake wa kutokuamini dini alizodai zililetwa na  wakoloni.

“Kaka huyu alikuwa na msimamo kweli kweli akiamua kitu akibadiliki” alisema Enock
Misimamo yake ilionekana kwenye ngazi za familia hadi Taifa ndio maana aliwai kufukuzwa kazi  Serikalini na Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere mwanzoni mwa  miaka ya 1970  kwa sababu alikataa kuunga mkono hoja ya mtu mmoja kuwa Mbunge,Waziri na Mkuu wa Mkoa.

Kingunge Ngombale-Mwiru alifariki Ijumaa wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha baada ya kuumwa na mbwa wake.

Ratiba ya mazishi
Jumatatu tarehe 5/2/2018
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili Karimjee Hall  kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini Kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani kwa chakula cha jioni
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli nzima.


No comments:

Post a Comment