Monday 20 June 2016

Hivi ndivyo UKAWA walivyotoka tena bungeni leo baada ya Naibu Spika Dk.Tulia kutangaza Ratiba ya shughuli ya Bunge(+picha).


Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo wametumia mtindo mpya kueleza hisia zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wamejifunika midomo kwa karatasi.


Hii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.




USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment