Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam imeyaondoa mashtaka mawili kati ya matano yanayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA Tundu Lisu pamoja na wenzake watatu katika mashtaka ya kuandika habari ya uchochezi kwenye gazeti la MAWIO ambalo limefutwa na serikali
Inadaiwa washtakiwa hao , Tundu Lissu , Simon Mkina , Ismail Menboob na Yusuph Abood, Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Wakili wa upande wa Jamhuri, Paul Kadushi,amemsomea Lisu Mashtaka ya uchochezi yanayomkabili baada ya awali kutokutokea mahakamani hapo wakati kesi ilipokuja kwa mara ya kwanza
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili PETER KIBATALA uliibua hoja za kisheria na kuitaka mahakama kufuta mashtaka mawili kwa madai kwamba yalikuwa hayaja ambatana na kibali cha mwanasheria mkuu wa serikali ambalo ni hitaji la kisheria , na kwakuwa vurugu hizo zingetokea zbar hivyo , mahakama ya kisutu haina mamlaka wa kusikiliza mashtaka hayo na pia maelezo ya kesi hayajitoshelezi.
USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment