Monday, 2 May 2016

Tazama jinsi wanafunzi 120 wanusurika kifo baada ya mabweni kuteketea kwa moto mkoani Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda
Zaidi ya wanafunzi 120 waliopo katika shule ya sekondari ya kikatiti wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamenusurika kifo,baada ya bweni wanalolitumia lenye vyuma tisa kuungia moto unaodaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme.

Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kikatiti, Tareto Nasari amesema tukio hilo la mto lilitokea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi wakijisomea lakini mpaka sasa chanzo tukio bado kinafanyiwa uchunguzi ingawa taarifa za awali zinasema ni hitilafu ya umeme.

Wakiongea katika eneo la tukio wanafunzi waliounguliwa na vifaa vyao wakati wa tukio hilo la mto wameiomba serikali kuwasaidia katika kipindi hiki kikugumu ili waendeele na masomo na kuomba hifadhi ya muda mpaka hapo serikali itakaporekebisha majengo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda, ameiagiza bodi ya shule kuhakikisha inafanya kazi bila kuathiri ratiba ya shule pamoja na mitahani inayoendelea.

Aidha Mmoja wa wadau wa elimu amewaomba wadau wengine wachangie shule hiyo ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo bila kuweka itikadi za kisiasa.

No comments:

Post a Comment