Monday 20 June 2016

Tazama listi yote ya Tetesi kubwa za usajili hii Leo hapa.

Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Napoli ya Italia Gonzalo Higuain (pichani) anayetajwa sana katika dirisha hili la majira ya kiangazi ya usajili.
Zifuatazo ni tetesi kubwa za usajili ambazo zimechukua nafasi kubwa:-
Gonzalo Higuain kutoka Napoli kwenda Atletico Madrid

Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya Taifa ya Argentina Gonzalo Higuain anatajwa kutaka kuhamia katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispani.

Hata hivyo mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid amesema kwa sasa atahitaji utulivu mpaka kumalizika kwa michuano ya Copa America inayorindima huko Marekani.

Pierre Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester City.
Licha ya kuwa kocha wa Klabu ya Manchester City Pep Guardiola kuhitaji huduma ya mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang, klabu hiyo haipo tayari kulipa kitita cha pauni milioni 65 kwa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Wakati huohuo klabu hiyo imetenga dau la pauni milioni 16.7 kwa ajili ya kumnyakua mshambuliaji wa Las Palmas ya Hispania Mbrazil Gabrieli Jesus ambaye pia anawaniwa na klabu za Manchester United na Bayern Munich.

Emanuele Giaccherini kutoka Sunderland kwenda Chelsea
Mshambuliaji Emanuele Giaccherini anayetikisa vilivyo na timu yake ya Taifa ya Italia amesema anataka kuungana na kocha Antonio Conte katika maisha yake mapya na klabu yake ya Chelsea.

Ramiro Funes Moro kutoka Everton kwenda Barcelona
Mabingwa wa La liga Fc Barcelona wanamfuatilia kwa karibu nyota wa Everton ya Uingereza Ramiro Funes Mori aliyeonekana kufanya vyema katika ligi kuu msimu uliopita


USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment