Thursday 9 June 2016

Wachambuzi wa Uchumi Watoa kauli hii kuhusu bajeti ya Serikali ya Rais Magufuli.

Wataalamu wa masuala ya uchumi nchini wamesema pamoja na bajeti ya serikali ya 2016/17 kuonyesha matumaini zaidi kuliko za miaka iliyopita,

 Bajeti hiyo haiweze kuleta unafuu wa maisha ya watanzania kwa muda mfupi, kutokana na mlengo wake wa kuangalia uwekezaji ambao unalenga zaidi kukuza viwanda vya ndani.
wataalamu wa masuala ya uchumi wamesema imekuwa na ubunifu zaidi ukilinganisha na ya miaka iliyopita, lakini pia imeongeza bajeti ya maendeleo ikimaanisha inawagusa wananchi zaidi, ingawa changamoto iliyopo ni namna ya kuhakikisha ukusanyaji wa kodi unaimarishwa ili fedha hizo ziweze kupatikana na hivyo miradi iliyopangwa iweze kutekelezeka.

Pamoja na kauli hizo za wachambuzi utafiti mwine unaonesha kuna baadhi ya  watanzania wengi ambao hawajui chochote kinachoendelea juu ya suala zima la bajeti, hali inayoonyesha kuwa pamoja na serikali kutengeneza bajeti hiyo ambayo inamlenga zaidi mwananchi  wa kawaida hivyo kuna uwezekano mkubwa wa miradi hiyo kukumbwa na changamoto katika utekelezaji wake na hivyo kutoleta matunda yaliyokusudiwa.

Katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2016/17 serikali imeongeza shilingi trioni saba zaidi ikilinganishwa na bajeti ya mwaka huu wa fedha na hivyo kufikia sh trillion 29.5, huku bajeti ya maendeleo ikiwa imeongezeka na kufikia asilimia arobaini, misamaha ya kodi kwenye taasisi mbalimbali imefutwa pamoja na kupunguza kodi kwenye nishati ya mafuta na kwenye mishahara ya wafanayakazi wa serikali.

No comments:

Post a Comment